• HABARI MPYA

    Saturday, March 28, 2015

    STARS TAYARI KUWAKABILI MALAWI KESHO CCM KIRUMBA

    Na Baraka Kizuguto, MWANZA
    TIMU ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) leo asubuhi imefanya mazoezi ya mwisho tayari kwa kuwakabili timu ya taifa ya Malawi (The Flames) mchezo utakaochezwa kesho jumapili saa 10.30 jioni katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
    Tiketi za mchezo tayari zimeshaanza kuuzwa katika vituo vya Uwanja wa Nyamagana na uwanja wa CCM Kirumba kwa bei za sh. 5,000 kwa mzunguko, sh. 12,000 kwa jukwaa kuu na sh.20,000 kwa viti vya jukwaa kuu maalum.
    Taifa Stars inashika nafasi ya 100 katika msimamo wa viwango vya FIFA vilivyotolewa mwezi Machi, huku Malawi (The Flames) wakishika wakiwa nafasi ya 91 kwenye vinago hivyo.

    Akiongea na waandishi wa habari leo kaika hoteli ya La Kairo iliyopo Kirumba jijini Mwanza, kocha msaidizi wa Taifa Stars Salum Mayanga amesema kikosi chao kipo katika hali nzuri , na sasa kilichobakia ni mchezo wenyewe wa kesho.
    Mayanga amesema vijana wake wote 22 waliopo kambini wapo fiti, wamefanya mazoezi kwa siku tano katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, wachezaji wapo kwenye ari na morali ya juu, kikubwa wanachosubiri ni kesho tu kushuka dimbani kusaka ushindi.
    Aidha Mayanga amewaomba wapenzi wa mpira wa miguu waliopo jijini Mwanza na mikoa ya jirani ya kanda ya ziwa, kujitokeza kwa wingi kesho uwanjani kuja kuwapa sapoti vijana kwa kuwashangilia muda wote wa mchezo.
    Tayari waamuzi na kamishina wa mchezo wameshawasili jijini Mwanza, mwamuzi wa kati atakua ni Munyazinza Gervais kutoka nchini Rwanda, akisaidiwa na mshika kibendera wa kwanza Hakizimana Ambroise (Rwanda), mshika kibendera wa pili Niyitegeka Bosco (Rwanda), mwamuzi wa akibaá Martin Saanya kutoka Morogoro huku na Kamishina wa mchezo ni Afred Rwiza kutoka Mwanza.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: STARS TAYARI KUWAKABILI MALAWI KESHO CCM KIRUMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top