• HABARI MPYA

    Wednesday, March 25, 2015

    NJEMBA LA SIMBA UKAWA LANASWA JANGWANI NDANI KABISA, YANGA WAMPELEKEA MTITI, POLISI WAJA KUMBEBA NA KARANDINGA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    MFUASI wa kundi la ‘Simba Ukawa’, wapinzani wa uongozi wa SImba SC chini ya Rais Evans Aveva, Hassan Msumari leo amenusurika kupigwa, baada ya kuvamia makao makuu ya klabu ya wapinzani, Yanga SC.
    Msumari aliyewahi kuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Chama cha Soka Temeke (TEFA), aliingia makao ya Yanga SC, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari.
    Hata hivyo, baadhi ya wanachama wakamshitukia na kumripoti, ndipo kundi la wanachama wachache wa klabu hiyo waliokuwapo klabuni lilipomvania kutaka kumpiga.
    Hassan Msumari akitolewa na Polisi makao makuu ya Yanga SC mchana wa leo


    Kulia Msumari anapandishwa kwenye karandinga, kushoto ameshapatiwa siti kwenye gari hilo

    Hata hivyo, busara ikatumika na kumuweka chini ya ulinzi kabla ya kupiga simu Polisi kumripoti. Baada ya dakika 20, Polisi walifika eneo la tukio na kumtia nguvuni Msumari na kuondoka naye kuelekea kiruo cha Polisi Msimbazi.
    Katika maelezo yake ya awali wakati amepewa kibano na makomandoo wa Yanga SC, Msumari alisema kwamba aifika hapo kwa ajili ya kuwafuata Waandishi wa Habari ili azungumze nao.
    Na akakiri ni mwanachama wa Simba mwenye kadi namba 4041 akitoka tawi la Tandika, na kwa sasa yeye ni Simba Ukawa, kikundi kinachoupinga uongozi uliopo madarakani.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NJEMBA LA SIMBA UKAWA LANASWA JANGWANI NDANI KABISA, YANGA WAMPELEKEA MTITI, POLISI WAJA KUMBEBA NA KARANDINGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top