• HABARI MPYA

    Sunday, March 01, 2015

    LIVERPOOL YAITANDIKA 2-1 MAN CIY ANFIELD

    LIVERPOOL imeichapa mabao 2-1 Manchester City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jioni ya leo Uwanja wa Anfield jioni ya leo.
    Jordan Henderson aliifungia bao la kwanza Liverpool dakika ya 11 kwa shuti la umbali wa mita 20 baada ya kazi nzuri ya Steven Gerrard.
    Edin Dzeko akafanikiwa kuisawazishia Man Cty dakika 15 baadaye, kabla ya Philippe Coutinho kuifungia bao la ushindi Liverpool dakika ya 75.
    Kipigo hicho kinaifanya Man City ibaki na poitni zake 55 za mechi 27, wakati Liverpool imafikisha pointi 48 za mechi 27.
    Kikosi cha Liverpool kilikuwa; Mignolet, Can, Skrtel, Lovren, Markovic/Sturridge dk76, Henderson, Allen, Moreno/KoloToure, Coutinho, Sterling na Adam Lallana.
    Man City; Hart, Zabaleta, Kompany, Mangala, Kolarov, Nasri/Lampard dk83, Toure, Fernandinho/Bony dk78), Silva, Aguero, Dzeko na Milner dk58.
    Coutinho is lost among a heap of his Liverpool team-mates as the Anfield side celebrate the Brazilian's winner against Manchester City
    Coutinho akipongezwa na wachezaji wenzake baada ya kuikfungia bao Liberpool leo

    PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2974376/Liverpool-2-1-Manchester-City-Philippe-Coutinho-wins-thriller.html#ixzz3T9ASeygn 

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: LIVERPOOL YAITANDIKA 2-1 MAN CIY ANFIELD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top