• HABARI MPYA

    Wednesday, January 21, 2015

    YANGA SC YAMFUNGULIA MASHITAKA BEKI WA RUVU ALIYEMNYANYASA AMISI TAMBWE

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    KLABU ya Yanga imepanga leo kuwasilisha malalamiko yao juu ya tukio la kunyanyaswa kwa mshambuliaji wake Amissi Tambwe kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lakini pia mchezaji husika amefafanua kwa kina juu ya manyanyaso anayoyapata.
    Akizungumza mchana huu katika makao makuu wa klabu hiyo Mkuu wa Kitengo cha Habari Jerry Muro amesema uongozi wao unakusudia kuwasilisha malalamiko yao hayo ambayo mengi yametokana na vitendo alivyofanyiwa Tambwe wikiendi iliyopita katika mchezo dhidi ya Ruvu Shooting ambapo wanataka mapendekezo yao manne yafanyiwe kazi.
    Amisi Tambwe (katikati) akiwa na Mkuu wa Idara ya Mawasiliano ya Yanga SC, Jerry Muro kulia na Mwanasheria wa klabu, Frank Chacha wakati wakizungumza na Waandishi wa Habari leo

    Muro amesema kwanza Yanga ingwetaka kuona TFF inawachukulia hatua kali wahusika wote waliomdhalilisha Tambwe huku pili wakilitaka shirikisho hilo kutoa hadharani taarifa ya tathimini ya waamuzi wa mchezo huo lengo likiwa ni kujua umakini wa waamuzi hao.
    "Tatu tungewaomba wenzetu wa TFF kwa kuwa wao wapo kimya pia kuwachukulia hatua wahusika wote waliosimamia mchezo huo kwa kushindwa kubaini haya ambayo vyombo vya habari imeyafichua lakini ikiwezekana wafungiwe na Yanga hatuwataki kuwaona wanachezesha mechi zetu vinginevyo tutagoma na hata Ruvu nao tungependa kuona wanapewa adhabu kwa viongozi wao kushabikia maovu haya.
    Amisi Tambwe chini, juu yake ni beki wa Ruvu Shooting, George Michael katika mchezo huo Jumamosi

    Aidha Tambwe mwenyewe amechukizwa na matukio hayo akisema ameshangazwa kuona anafanyiwa vitendo vya kinyama ambapo mengine hawezi kuyaweka hadharani.
    "Mpira ni starehe mimi sikatai mchezaji anikabe lakini ni jinsi gani unanikaba hapo ndiyo tatizo, naambiwa mimi mkimbizi hivi hawa wenzangu wanajua maana na haya maneno yapo mengi ambayo nimedhalilishwa nayo kiungwana siwezi kuyaweka wazi hapa lakini viongozi nitawaeleza,"alisema Tambwe.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA SC YAMFUNGULIA MASHITAKA BEKI WA RUVU ALIYEMNYANYASA AMISI TAMBWE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top