• HABARI MPYA

    Saturday, January 31, 2015

    ILIVYO NGUMU MAN CITY KUSHINDA MECHI BILA YAYA TOURE, CHELSEA KUJILIA PWEZA KIZANI LEO?

    KLABU ya Chelsea itawakosa nyota wake Diego Costa na Cesc Fabregas katika mechi ya Ligi Kuu ya England dhidi ya Manchester City leo, lakini Manuel Pellegrini amekuwa akichezea vipigo siku za karibuni.
    Mabingwa hao wa Ligi Kuu hawajaweza kushinda mechi tangu kiungo Yaya Toure aende kwenye Fainali za Mataifa ya Afrika mwezi huu na watamkosa Mwanasoka huyo Bora wa Afrika leoUwanja wa Stamford Bridge. 
    Ikiwa na Toure kikosini, City imeshinda mechi 14 kati ya 18 za Ligi Kuu, ikipoteza moja na kutoa sare tatu kati ya mechi nne ambazo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 alizokosa.
    Manchester City are yet to win a game since Yaya Toure's departure for the 2015 Africa Cup of Nations
    Manchester City haijashinda mechi tangu Yaya Toure ameondoka Fainali za Mataifa ya Afrika
    Toure's Ivory Coast are through to the AFCON quarter-finals and will face Algeria
    Timu ya Toure, Ivory Coast imeingia Robo Fainali za AFCON na itamenyana na Algeria
    MECHI AMBAZO MAN CITY ILIMKOSA TOURE
    Ikiwa na ToureLigi Kuu 2014-15Bila Toure
    18Mechi4
    14Kushinda0
    2Sare3
    2Kufungwa1
    40Mabao iliyofunga5
    2.2Wastani mabao ya
    kufunga 
    1.2
    15Mabao waliyofungwa7
    0.8Wastani wa mabao 
    ya kufungwa 
    1.8
    77.8%Asilimia ya ushindi0.0%
    2.4Pointi/Mechi0.8

    Licha ya kuendelea kwa tetesi za kuondoka Etihad, Toure anabaki kuwa mtu muhimu katika safu ya kiuno ya City, baada ya kuiongoza vyema timu yake na kupata mabao muhimu- tayari ana mabao tisa msimu huu.
    Lakini kwa timu ya Toure, Ivory Coast kwenda Robo Fainali za AFCON, kuna nafasi finyu ya mchezaji huyo wa zamani wa Barcelona kurejea kazini City kabla ya katikati ya February kwa sababu Tembo wana nafasi ya kwenda hadi Fainali.
    Pellegrini atatumai kwamba Toure na mchezaji mpya, Wilfried Bony watarejea England mapema zaidi, hivi sasa timu yake ikiwa inazidiwa pointi tano na vinara, Chelsea.
    Chelsea could also be without Diego Costa, who is facing a three-match ban for violent conduct
    Chelsea pia itamkosa Diego Costa, ambaye amefungiwa mechi tatu kwa kucheza rafu

    Tangu kiungo huyo amekwenda Equatorial Guinea mapema Januari, City imefungwa mabao 2-0 katika Kombe la FA na Middlesbrough na pia ikafungwa na timu ya Arsene Wenger, Arsenal. 
    Ikiwa na Toure kikosini, wimbi la ushindi la City linakwenda hadi asilimia 80, pamoja na wastani wa mabao 2.2 ya kufunga ukilinganisha na wastani wa 1.8 anapokosekana.
    Pellegrini anafahamu City inakuwa katika mgumu sana inapomkosa Toure na bila shaka anachoomba na kiungo huyo kurejea mapema.
    Manuel Pellegrini's side will fall eight points behind Chelsea if they lose at Stamford Bridge on Saturday
    Manuel Pellegrini amekuwa na wakati mgumu anapomkosa Yaya Toure, na lkeo hatakuwa naye Uwanja wa Stamford Bridge akimenyana na wenyeji, Chelsea
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ILIVYO NGUMU MAN CITY KUSHINDA MECHI BILA YAYA TOURE, CHELSEA KUJILIA PWEZA KIZANI LEO? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top