URA wameng'ara jana Uganda |
Ushindi huo unawafanya Watoza kodi hao washinde mechi ya saba na ya tatu mfululizo, hivyo kufikisha pointi 23 na kujikita nafasi ya nne.
Kwa Tai Wekundu wanashuka kwa nafasi moja hadi ya saba wakibaki na pointi zao 21 baada ya mechi 14. Mchezo mwingine jana mabingwa watetezi, KCC wamefungwa 1-0 na Lweza Uwanja wa Wankulukuku.
Entebbe nayo ilishinda mechi yake ya pili jana UPL baada ya kuwachapa Rwenshama 2-1 Uwanja wa Nakivubo. Ali Adam na Hussein Mubiru walifunga mabao ya Entebbe, wakati Farouk Kalinzi aliwafungia wageni la kufutia machozi.
Mabao mawili ya Umar Kasumba yameipa ushindi wa 2-0 Polisi dhidi ya Soana Uwanja wa Kavumba.
0 comments:
Post a Comment