• HABARI MPYA

    Friday, December 19, 2014

    SIMBA SC YA AVEVA YAANZA MCHAKATO UJENZI WA COMPLEX LA MAANA BUNJU, YASEMA ITATUMIA BILIONI 2. 5

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KLABU ya Simba imeingia mkataba na kampuni ya uchoraji ramani ya Envirolink ili iweze kuwapatia michoro ya hosteli na namna ya kuendeleza mradi wa Bunju ambao utaigharimu Simba zaidi ya Sh 2.5 bilioni hadi kukamilika kwake.
    Rais wa Simba, Evans Aveva amesema kuwa kampuni ya Envirolink tayari imewakwisha wasilisha  michoro ya mradi huo na kuwa matarajio ni kuwa shughuli hiyo itaanza mapema iwezekanavyo.
    Rais wa SImba SC, Evans Aveva akizungumza na Waandishi wa Habari leo Msimbazi

    "Tayari kuna mengi yaliyofanyika, kwanza ninapenda kutoa pongezi  kwa wanachama wa baadhi ya matawi kama ya Wazo Hill na tawi la Platinum ambao wanachangia Tani 10 za sementi na matofali 1000 kwa ajili ya mradi huo. Ni imani yetu kuwa wazee wetu waliweza kujenga kwa nguvu zao wenyewe makao makuu yetu pale Msimbazi, Kariakoo jijini Dar es Salaam, na sisi hatuna shaka kizazi hiki kitajenga mradi huu wa Bunju," alisema Aveva.
    Rais Aveva amesema kuwa muendeno wa timu ya Simba hadi sasa haiendani na hadhi ya klabu hiyo na hivyo wamefanya mabadiliko mengi baada ya kugundua matatizo.
    Aveva alisema, " Tuligundua kuwa sababu zilizokuwa zikituangusha ni uwepo wa timu changa, ugeni wa kocha Patrick Phiri  lakini pia ugeni wa viongozi wengi kwenye soka.
    "Nafasi tuliopo haiendani na hadhi, uzoefu na ukongwe wetu kwenye ligi lakini sasa naamini kuna mengi yanafanyika ikiwemo kumpa kocha nafasi ya kufanya baadhi ya mabadiliko yakiwemo kwenye usajili," alisema.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC YA AVEVA YAANZA MCHAKATO UJENZI WA COMPLEX LA MAANA BUNJU, YASEMA ITATUMIA BILIONI 2. 5 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top