• HABARI MPYA

    Wednesday, October 01, 2014

    WELBECK APIGA HAT TRICK ARSENAL IKIUA 4-1 ULAYA, RONALDO AING’ARISHA REAL KWA TUTA

    MSHAMBULIAJI Danny Welbeck amefunga hat trick yake ya kwanza Arsenal ikishinda 4-1 katika mchezo wa Kundi D Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku huu Uwanja wa Emirates. 
    Mshambuliaji huyo aliyenunuliwa kutoka Manchester United msimu huu, alifunga mabao hayo katika dakika za 22, 30 na 52 wakati lingine limefungwa na Alexis Sanchez dakika ya 41- huku bao la wageni likifungwa na Burak Yilmaz kwa penalti dakika ya 63.
    Kipa wa Arsenal, Szcezesny alitolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 60 na bado hiyo haikuizuia timu ya Arsene Wenger kushinda.

    Ni mimi; Danny Welbeck akishangilia baada ya kupiga hat trick Arsenal ikishinda 4-1 usiku huu

    Mchezo mwingine wa Kundi D, Anderlecht imechapwa 3-0 nyumbani na Borrusia Dortmund mabao ya Ciro Immobile dakika ya tatu na Adrian Ramos dakika ya 69 na 79.
    Kundi A bao pekee la Ada Turan limetosha kuipa Atletico Madrid ushindi wa 1-0 dhidi ya Juventus wakati katika mchezo mwingine wa kundi hilo, Malmo FF ya Sweden imeichapa 2-0 Olympiacos ya Ugiriki mabao yake yakitiwa kimiani na M Rosenberg dakika ya 42 na 82.
    Kundi B, Basel imeichapa 1-0 Liverpool bao pekee la Marco Streller dakika ya 52, wakati Real Madrid imeshinda ugenini mabao 2-1 dhidi ya PFC Ludogorets Razgrad.
    Wenyeji walitangulia kupata bao dakika ya sita kupitia kwa Marcelinho kabla ya Cristiano Ronaldo kufunga kwa penalti dakika ya 25 na Karim Benzema kufunga la ushindi dakika ya 77.
    Katika Kundi C, Zenit St Petersburg imetoka 0-0 na Monaco huku Bayer Leverkusen ikiitandika 3-1 Benfica, mabao ya Stefan Kiessling dakika ya 25, Heung-Min Son dakika ya 34 na Calhanoglu dakika ya 64, huku Eduardo Salvio akiwafungia Benfica dakika ya 62.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WELBECK APIGA HAT TRICK ARSENAL IKIUA 4-1 ULAYA, RONALDO AING’ARISHA REAL KWA TUTA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top