• HABARI MPYA

    Thursday, October 02, 2014

    RONALDO BADO MABAO MAWILI TU KUMKAMATA RAUL LIGI YA MABINGWA, MESSI ATUPWA HUKO!

    BADO mabao mawili tu Cristiano Ronaldo afikie idadi ya mabao ya Raul anayeongoza kwa kufunga zaidi kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya. 
    Ronaldo usiku huu amezidi 'kuisuuza roho' ya kocha wake, Carlo Ancelotti baada ya kufunga bao moja katika ushindi wa 2-1 ugenini dhidi ya PFC Ludogorets Razgrad.
    Wenyeji walitangulia kupata bao dakika ya sita kupitia kwa Marcelinho kabla ya Cristiano Ronaldo kufunga kwa penalti na Karim Benzema kufunga la ushindi kwa Real Madrid.
    Mfalme wa mabao; Nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amebakiza bao moja kufikia rekodi ya Raul katika Ligi ya Mabingwa Ulaya

    WAFUNGAJI BORA WA KIHISTORIA LIGI YA MABINGWA UALAYA 

    1. Raul - Mabao 71 
    2. Cristiano Ronaldo - Mabao 69
    2= Lionel Messi - Mabao 68
    4. Ruud van Nistelrooy - Mabao 56
    5. Thierry Henry - Mabao 50
    6. Alfredo Di Stefano - Mabao 49
    7. Andriy Shevchenko - Mabao 48
    8. Eusebio - Mabao 46
    8= Filippo Inzaghi - Mabao 46 
    10. Didier Drogba - Mabao 42 
    Mwanasoka huyo bora wa dunia sasa anatimiza mabao 69 aliyofunga katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, mawili nyuma ya Raul aliyefunga mara 71.
    Anafunga bao hilo siku moja baada ya kocha Ancelotti kukaririwa akisema "Ni mchezaji bora zaidi niliyewahi kumfundisha,".
    Kipenzi huyo wa mashabiki wa Manchester United sasa anamzidi kwa bao moja, mpinzani wake Lionel Messi wa Barcelona, ambaye ana mabao 68. Ruud van Nisterlooy anashika nafasi ya nne kwa mabao yake 56, Thierry Henry mwenye mabao 50 ni wa tano, Alfred de Stefano mwenye mabao 49 ni wa sita, Andriy Shevchenko mwenye mabao 48 ni wa saba, wakati Eusebio mwenye mabao 46 sawa na Filippo Inzaghi wanashika nafasi ya nane. Didier Drogba anakamilisha orodha ya wachezaji 10 waliofunga mabao mengi Ligi ya Mabingwa kwa mabao yake  42.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RONALDO BADO MABAO MAWILI TU KUMKAMATA RAUL LIGI YA MABINGWA, MESSI ATUPWA HUKO! Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top