• HABARI MPYA

    Monday, October 20, 2014

    MCHEZAJI AFARIKI LIGI KUU INDIA AKIJARIBU KUSHANGILIA BAO KAMA KLOSE

    MWANASOKA amefariki dunia baada ya kuanguka vibaya aliporuka samasoti kushangilia bao katika mchezo wa Ligi Kuu ya jimbo la Mizoram nchini India.
    Peter Biaksangzuala amefariki akiwa hospitali Jumapili baada ya kuangukia kichwa chake aliporuka samasoti kushangilia bao aliloifungia Bethlehem Vengthlang FC - klabu yenye maskani yake Kaskazini Mashariki kwa jimbo la Mizoram.
    Mchezaji huyo aliyekuwa ana umri wa miaka 23 alifunga bao hilo dakika ya 62 kuisawazishia timu yake dhidi ya Chanmari West FC Jumanne katika mchezo wa Ligi na akataka kushangilia kwa staili ya mfungaji bora wa kihistoria wa Kombe la Dunia, Miroslav Klose.

    Peter Biaksangzuala (aliyezungushiwa duara kulia) amefariki dunia baada ya kuumia akishangilia bao
    Biaksangzuala wheels away in celebration after scoring the equaliser against Chanmari West FC
    Biaksangzuala akikimbia kwenda kushangilia bao lake dhidi ya Chanmari West FC
    The 23-year-old attempted a somersault celebration in the Indian Mizoram Premier League match
    The midfielder's celebration (ringed bottom) goes horribly wrong as he lands on his head in Tuesday's match
    Biaksangzuala alikosea katika kuruka kwake na akapigiza kichwa chini, kabla ya kupatiwa huduma ya kwanza uwanjani na kisha kutolewa nje kwa machela.
    Biaksangzuala alikimbizwa katika hospitali ya Aizawl Civil ambako vipimo vya CT vilionyesha amepata madhara makubwa kwa undani na mara moja akahamishiwa chumba cha wagonjwa walio chini ya uangalizi maalum.
    Chanzo kimesema: "Alijaribu kushangilia kama Mjerumani Klose, lakini akakosea kwa bahati mbaya. Alikaa hospitali kwa siku tano, lakini madaktari hawakufanikiwa kuokoa uhai wake,".
    Taarifa nchini India zinasema kwamba Biaksangzuala alichangia macho yake wakati akiwa amelazwa hospitali.
    Kwa ajili ya kumbukumbu ya kiungo huyo, Bethlehem Vengthlang FC imeamua kuipumzisha jezi namba 21 na Chama cha Soka Mizoram kimetoa taarifa katika Ukurasa wake maalum wa Facebook.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MCHEZAJI AFARIKI LIGI KUU INDIA AKIJARIBU KUSHANGILIA BAO KAMA KLOSE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top