• HABARI MPYA

    Monday, October 20, 2014

    CANNAVARO ATOLEWA NYUZI ALIZOCHEZEA DHIDI YA SIMBA JUMAMOSI

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    BEKI wa Yanga SC, Nadir Haroub Ali ‘Cannavaro’ leo ametolewa nyuzi tatu alizoshonwa chini ya jicho la kulia, baada ya kuumia akiichezea timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars.
    Cannavaro aliumia Oktoba 12, akiichezea Stars dhidi ya Benin katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa, ambao alifunga bao moja katika ushindi wa 4-1.
    Nahodha huyo wa Yanga SC licha ya kumalizia mchezo huo, lakini baada ya mechi akaenda kufanyiwa tiba hiyo yA kuzibwa jeraha lake.
    Nadir Cannavaro ametolewa nyuzi alizoshonwa baada ya kuumia akiichezea Taifa Stars dhidi ya Benin

    Akiwa na nyuzi zake hizo, Cannavaro aliichezea klabu yake, Yanga SC ikitoka sare ya 0-0 na mahasimu wao, Simba SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Cannavaro aliyefanyiwa tiba hiyo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam amedumu na nyuzi hizo kwa siku tano tangu ashonwe na sasa anaweza kuendelea na kazi akiwa vizuri kabisa.
    Baada ya sare hiyo ya Jumamosi, Yanga SC inatarajiwa kushuka tena dimbani Jumamosi ijayo Uwanja wa Kambarage, Shinyanga dhidi ya wenyeji Stand United. 
    Mwenendo wa Yanga SC katika Ligi Kuu hadi sasa si wa kuridhisha sana, ikiwa ina pointi saba baada ya mechi nne, kutokana na sare moja, kufungwa moja na kushinda mbili- hivyo kuzidiwa kwa pointi tatu na Azam FC na Mtibwa Sugar walio kileleni kwa pointi zao sawa, 10. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CANNAVARO ATOLEWA NYUZI ALIZOCHEZEA DHIDI YA SIMBA JUMAMOSI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top