• HABARI MPYA

    Tuesday, September 02, 2014

    VITA YA NAMBA NJE NJE MAN UNITED, VAN PERSIE NAYE AMKARIBISHA NA MANENO FALCAO; "NJOO TUGOMBEE KUCHEZA"

    MSHAMBULIAJI Robin van Persie amepuuzia madai kwamba matatizo yake ya goti ndiyo yameifanya Manchester United imsajili Radamel Falcao, na amesema anajiandaa kufanya kazi na mkali huyo mpya.
    Iliripotiwa kwamba kocha Louis van Gaal alikuwa anahofia majeruhi ya Mholanzi mwenzake huyo kama angehitaji upasuaji na ndiyo maana akatoa Pauni Milioni 6 kumsajili Falcao kwa mkopo, lakini Van Persie amesema maneno hayo hayana maana hata kidogo na atapambana kupata nafasi ya kucheza na Mcolombia huyo.

    Washirika watatu: Van Gaal atalazimika kuumiza kichwa katika kuipanga safu yake ya ushambuliaji msimu huu

    "Inanifurahisha watu wanavyotengeneza maneno ya uzushi namna hii. Sijui yanatoka wapi na naweza kusema na mono wangu ukiwa moyoni mwangu kwamba sitakwenda kufanyiwa upasuaji hospitali.
    Falcao atavaa jezi namba 9 Old Trafford baada ya kusajiliwa kwa mkopo kutoka Monaco na mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28 atakuwa analipwa kiasi cha Pauni 280,000 kwa wiki.
    Na katokana na rekodi yake nzuri ya kufunga mabao ukilinganisha na kwamba Wayne Rooney ameteuliwa kuwa Nahodha wa timu, inafikiriwa Van Persie atasotea namba kikosi cha kwanza. Lakini mshambuliaji huyo wa zamani wa Arsenal amesema anakaribisha ushindani wa namba.
    "Nakaribisha ujio wake, atatufanya tube bora. Katika klabu kubwa lazima wakati wote uwe na wachezaji bora, ambayo pia ndiyo falsafa yangu. Falcao lazima apiganie nafasi yake, nami pia kadhalika. Lazima tupambane na Wayne Rooney na James Wilson kuona nani watacheza.
    Van Persie ameukosa mwanzo wa msimu baada ya kupewa mapumziko kufuatia kumalizika kwa Kombe la Dunia, lakini alicheza kwa dakika 60 dhidi ya Burnley mwishoni mwa wiki.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: VITA YA NAMBA NJE NJE MAN UNITED, VAN PERSIE NAYE AMKARIBISHA NA MANENO FALCAO; "NJOO TUGOMBEE KUCHEZA" Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top