• HABARI MPYA

    Tuesday, September 02, 2014

    ROONEY AMTUNISHIA KIFUA FALCAO VITA YA NAMBA MAN UNITED

    MSHAMBULIAJI Wayne Rooney amefurahia klabu yake Manchester United's kumsajili Radamel Falcao akisema ni mchezaji mzuri, lakini amesema hahofii kupokonywa namba.
    Usajili wa Falcao ndio lilikuwa tukio kubwa zaidi katika siku ya kufungwa pazia la usajili, nyota huyo wa Colombia akitua United kwa mkopo wa Pauni Milioni 6 kutoa huduma kikosi cha Louis van Gaal.
    Lakini Nahodha huyo wa United na England, Rooney hahofii ujio wa mchezaji huyo kuhusu nafasi yake kikosini humo na anatarajia kucheza naye.

    Hana hofu: Wayne Rooney anatumai ujio wa Radamel Falcao Manchester United ni jambo zuri
    Pose: Radamel Falcao holds his Manchester United jersey aloft after completing a season-long loan move
    Pozi: Radamel Falcao akiwa ameshika jezi ya Manchester United baada ya kukamilisha uhamisho wake jana

    Akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari kuelekea mchezo wa kirafiki wa England dhidi ya Norway, Rooney amesema: "Sijui itaathiri vili nafasi yangu, unatakiwa kumuuliza kocha,"alisema Rooney na kuongeza. 
    "Nafikiri ni usajili mzuri kwa kuwa ni mmoja wa wachezaji bora duniani," .
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ROONEY AMTUNISHIA KIFUA FALCAO VITA YA NAMBA MAN UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top