• HABARI MPYA

    Saturday, September 20, 2014

    NDANDA FC WA BIN SLUM WAANZIA KILELENI LIGI KUU BARA, WATISHIA AMANI AZAM FC

    WAGENI wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Ndanda FC wameanzia kileleni kufuatia ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya wenyeji Stand United Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.

    MATOKEO MECHI ZA UFUNGUZI LIGI KUU YA VODACOM TZ BARA LEO

    Azam FC 3-1 Polisi Moro
    Stand Utd 1-4 Ndanda FC
    Mgambo 1-0 Kagera Sugar
    Ruvu Shooting 0-2 Prisons 
    Mtibwa Sugar 2-0 Yanga 
    Mbeya City 0-0 JKT Ruvu
    Maana yake, Ndanda wanaodhaminiwa na kampuni ya Bin Slum pamoja na Mbeya City na Stand United, wanakuwa wanaongoza msimamo wa Ligi Kuu kwa wastani wa mabao, wakifuatiwa na mabingwa watetezi, Azam FC walioshina 3-1 dhidi ya wageni wengine kwenye ligi hiyo, Polisi Morogoro. 
    Mtibwa Sugar iliyoifunga mabao 2-0 Yanga SC Uwanja wa Jamhuri, Morogoro ipo nafasi ya tatu sawa na Prisons ya Mbeya iliyowachapa wenyeji Ruvu Shooting mabao 2-0, wakati JKT Mgambo 1-0 iliyoilaza Kagera Sugar 1-0 ipo chini yao. 
    Mbeya City iliyolazimishwa sare ya 0-0 na JKT Ruvu Uwanja wa Sokoine, Mbeya iko juu ya Yanga SC iliyolala 2-0 na timu nyingine zote zilizopoteza mechi leo.
    Ligi Kuu itaendelea kesho kwa mchezo mmoja kati ya Coastal Union ya Tanga dhidi ya wenyeji Simba SC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Udhamini mnono na ushindi; Mkurugenzi wa kampuni ya Bin Slum, Nassor Bin Slum kulia akimkabidhi vifaa kiongozi wa Ndanda kushoto wakati wa kutangaza kuidhamini timu hiyo mpya ya Ligi Kuu
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NDANDA FC WA BIN SLUM WAANZIA KILELENI LIGI KUU BARA, WATISHIA AMANI AZAM FC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top