• HABARI MPYA

    Sunday, September 21, 2014

    MAZEMBE WAPIGWA 2-1 SETIF, REFA AWAPA WAARABU BAO TATA, SAMATTA AKOSA BONGE LA BAO ALGERIA

    Na Salum Ezry, SETIF
    TP Mazembe imefungwa mabao 2-1 usiku wa kuamkia leo katika Nusu Fainali ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika na wenyeji ES Setif mjini Setif nchini Algeria.
    Shukrani kwake Abdelmalek Ziaya aliyeifungia Entente Setif bao la ushindi dakika za lala salama, wengi wakiamini mechi itaisha 1-1. 
    Timu hizo zilikwenda kupumzika zikiwa hazijafungana huku mshambuliaji Mtanzania wa Mazembe, Mbwana Samatta akikosa bao la wazi baada ya kuunganishia juu ya lango krosi ya winga wa Ghana, Solomon Asante dakika ya 30.
    Mazembe walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 51 baada ya beki wa Setif, Said Aroussi kujifunga katika jitihada za kuokoa krosi ya Rainford Kalaba.
    TP Mazembe sasa itahitaji ushindi wa 1-0 nyumbani kwenda Fainali

    Dakika mbili baadaye, Setif ilisawazisha kwa bao la utata wakati Younes alipounganisha krosi ya Ali Lamri akiwa ameotea.
    Hata hivyo, utata ulitokana na refa Neant Alioum kukubali bao hilo, huku mshika kibendera wake akisema mfungaji alikuwa ameotea.
    Baada ya kuzongwa na wachezaji wa Setif, Alioum akalikubali bao hilo na Mazembe wakaendelea kusukuma mashambulizi langoni mwa 
    Setif, lakini kwa bahati mbaya wakaishia kukosa mabao.
    Ikiwa imebaki dakika mmoja mchezo kumalizika, Ziaya akaifungia bao la ushindi Setif baada ya kumtoka beki wa Zambia, Chongo Kabaso kabla ya kumtungua kipa Robert Kidiaba.
    Timu hizo mbili zitarudiana Septemba 27 mjini Lubumbashi kutafuta timu ya kwenda fainali, Mazembe ikihitaji ushindi wa 1-0 nyumbani ili kusonga mbele. Fainali zinatarajiwa kufanyika wikiendi ya Oktoba 25 na 26 na marudiano Novemba 1 na 2.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAZEMBE WAPIGWA 2-1 SETIF, REFA AWAPA WAARABU BAO TATA, SAMATTA AKOSA BONGE LA BAO ALGERIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top