• HABARI MPYA

    Sunday, September 21, 2014

    MAN UNITED YAPIGWA 5-3 NA LEICESTER, MASTAA WOTE WA PAUNI MILIONI 150 WAKIWEPO UWANJANI

    MANCHESTER United imechapwa mabao 5-3 na Leicester City ugenini jioni hii katika mchezo wa Ligi Kuu ya England, mshambuliaji Radamel Falcao akianza kwa mara ya kwanza tangu ajiunge na Mashetani hao Wekundu kwa mkopo kutoka Monaco.
    Robin van Persie aliifungia United bao la kuongoza dakika ya 13 akiunganisha krosi ya Falcao kabla ya
    Angel di Maria kufunga la pili dakika tatu baadaye.
    Leonardo Ulloa akaifungia Leicester bao la kwanza kabla ya Ander Herrera kuifungia la tatu United.
    David Nugent akaifungia bao la pili Leicester kwa penalti ya utata iliyotolewa dhidi ya Rafael na Esteban Cambiasso akafunga la tatu dakika ya 63.
    ‘Kifo’ cha Man United leo inayofundishwa na Mholanzi, Louis Van Gaal aliyetumia Pauni Milioni 150 kusajili kilikamilishwa na Jamie Vardy aliyeifungia bao la nne Leicester zikiwa zimebaki dakika 12 na Ulloa aliyefunga la tano kwa penalti iliyosababishwa na Tyler Blackett ambaye alitolewa nje kwa adi nyekundu.
    Kikosi cha Leicester kilikuwa: Schmeichel, De Laet, Morgan, Moore, Konchesky, Hammond, Drinkwater, Cambiasso/King, Nugent/James, Ulloa nja Vardy/Schlupp.
    Man Utd: De Gea, Da Silva, Evans/Smalling, Blackett, Rojo, Blind, Ander Herrera, Di Maria/Mata, Rooney, Falcao/Januzaj na Van Persie.

    Mshambuliaji wa Man United, Falcao akimtoka Ritchie De Laet wa Leicester leo
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAN UNITED YAPIGWA 5-3 NA LEICESTER, MASTAA WOTE WA PAUNI MILIONI 150 WAKIWEPO UWANJANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top