• HABARI MPYA

    Tuesday, September 02, 2014

    FALCAO ALIVYOTAMBULISHWA MANCHESTER UNITED

    KLABU ya Manchester United imemtambulisha rasmi mshambuliaji Radamel Falcao baada ya kukamilisha uhamisho wake katika siku ya mwisho ya kufungwa pazia la usajili.
    Mpachika mabao huyo wa Monaco aria wa Colombia aliwasili kwa ndege binafsi kusaini mkataba wa mkopo wa muda mrefu wa msimu Old Trafford kwa ada ya Pauni Milioni 6, ambao unatoa fursa ya kununuliwa moja kwa moja kwa Pauni Milioni 46.
    Falcao ameiambia www.manutd.com: "Nina furaha kujiunga na Manchester United kwa mkopo msimu huu. Manchester United ni klabu kubwa duniani na wazi inatakiwa kurudi juu,"amesema mchezaji huyo ambaye ameweka wazi hamu yake ya kufanya kazi na kocha Louis van Gaal ili kutoa mchango wake kuirudisha juu klabu hiyo.
    Pozi: Radamel Falcao akiwa ameshika jezi ya Manchester United baada ya kukamilisha uhamisho wake wa mkopo wa muda mrefu usiku wa kuamkia leoSide by side: Falcao poses with the United shirt and assistant manager Ryan Giggs
    Falcao akiwa ameshika kwa pamoja jezi ya United na kocha Msaidizi wa timu hiyo, Ryan GiggsSide by side: Falcao poses with the United shirt and assistant manager Ryan Giggs
    Nyota huyo wa Colombia anakuwa mchezaji wa nane kutoka nchi hiyo kucheza Ligi Kuu ya England
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: FALCAO ALIVYOTAMBULISHWA MANCHESTER UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top