• HABARI MPYA

    Tuesday, September 02, 2014

    BEK LA MAN CITY LAHAMIA SERIE A KWA MKOPO

    BEKI Micah Richards amejiunga na Fiorentina kwa mkopo wa muda mrefu wa msimu baada ya West Ham kushindwa kumsajili mchezaji huyo wa Manchester City.
    Richards, mwenye umri wa miaka 26, amesaini klabu hiyo ya Serie A baada ya Hammers kushindwa kumlipa mshahara wake wa Pauni 75,000 kwa wiki.
    City pia imepata Pauni Milioni 1 ya ada ya mkopo baada ya West Ham kugoma kumnunua mchezaji huyo wakati uhamisho wa Fiorentina ni wa muda ingawa kuna fursa ya kuuziana moja kwa moja beki huyo.
    Maisha mapya; Micah Richards ametua Italia kujaribu kufufua makali yake baada ya mambo kumuendea ndivyo sivyo Man City 
    Arrival: Micah Richards pictured after landing in Florence on Monday morning to seal his loan move
    Alipowasili: Micah Richards pichani baada ya kuwasili Florence jana asubuhi kukamilisha uhamisho huo wa mkopo
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BEK LA MAN CITY LAHAMIA SERIE A KWA MKOPO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top