• HABARI MPYA

    Sunday, September 21, 2014

    AZAM FC NA POLISI MORO KATIKA PICHA JANA CHAMAZI

    Kiungo wa Azam FC, Salum Abubakar 'Sure Boy' akimtoka beki wa Polisi Moro katika mchezo wa ufunguzi Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jana, Azam FC ilishinda 3-1
    Mshambuliaji wa Azam FC, Didier Kavumbangu akiteleza kuunganisha krosi ya Kipre Tchetche (hayupo pichani) kuifungia Azam FC bao la kwanza kati ya mawili aliyofunga jana kwenye ushindi wa 3-1
    Kipre Tchetche akitafuta maarifa ya kumtoka beki wa Polisi Moro
    Kiungo wa Azam FC, Mudathir Yahya akijaribu kupasua katikati ya wachezaji wa Polisi
    Himid Mao wa Azam FC akiugulia maumivu ya kuchezewa rafu na mchezaji wa Polisi kulia
    Kiungo mkongwe wa Polisi, Bantu Admin akimtoka kiungo wa Azam FC, Himid Mao kushoto
    Beki chipukizi wa Azam FC, Gardiel Michael akimdhibiti mshambuliaji mkongwe wa Polisi, Danny Mrwanda kushoto
    Beki wa Azam FC, Aggrey Morris katikati ya kipa na beki wa Polisi akijaribu kufunga. Aggrey alifunga bao moja katika ushindi wa 3-1

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC NA POLISI MORO KATIKA PICHA JANA CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top