• HABARI MPYA

    Tuesday, August 19, 2014

    SUAREZ AANZA KAZI RASMI BARCELONA IKIUA 6-0 NA KUTWAA KOMBE

    MSHAMBULIAJI Luis Suarez jana ameichezea kwa mara ya kwanza timu yake mpya, Barcelona ikishinda mabao 6-0 Uwanja wa Camp Nou dhidi ya FC Leon, baada ya kupunguziwa adhabu na CAS.
    Suarez alifungiwa kujihusisha kabisa na soka kwa miezi minne baada ya kumng'ata Giorgio Chiellini wa Italia kwenye Kombe la Dunia, lakini CAS inapunguza makali yake ya soka kwa kumruhusu kufanya mazoezi na kucheza mechi zisizo za mashindano za Uruguay na Barcelona.
    Na jana akaingia kuchukua nafasi ya Rafinha dakika ya 76, wakati huo tayari Barca inaongoza 4-0. 
    Ameanza kazi: Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool, Luis Suarez aliyetua kwa Pauni Milioni 75 Barcelona jana ameanza kazi Camp Nou

    Messi alifunga dakika ya tatu kwa pasi ya Neymar ambaye alifunga dakika ya 12 baada ya pasi nzuri ya Andres Iniesta. Neymar akafunga la tatu, dakika mbili kabla ya mapumziko baada ya kuvunja mtego wa kuotea wa FC Leon kufuatia pasi ya Messi. Mbrazil huyo alitolewa nje baada ya dakika 45 akimpisha El Haddadi Munir. 
    Still got it! Lionel Messi sets the tone by taking on the Leon defence in the opening minutes
    Lionel Messi akiipangua safu ya ulinzi ya Leon 
    Double act: Lionel Messi celebrates with Neymar after the Brazilian set up the first goal
    Lionel Messi akishangilia na Neymar baada ya Mbrazil huyo kufunga
    Boy from Brazil: Neymar looked sharp as he doubled Barcelona's lead in the first-half
    Neymar aliranya vitu vya uhakika jana
    Championes: Veteran midfielder Xavi holds up the Gamper Cup following the 6-0 demolition
    Kungo Xavi akiwa ameshika Kombe la Gamper baada ya ushindi wa 6-0
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SUAREZ AANZA KAZI RASMI BARCELONA IKIUA 6-0 NA KUTWAA KOMBE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top