• HABARI MPYA

    Tuesday, August 19, 2014

    KOZI YA UKOCHA LESENI A KUFANYIKA SEPTEMBA 4

    Na Boniface Wambura, DAR ES SALAAM
    KOZI ya ukocha wa Leseni A inayotambuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) itafanyika mara ya kwanza nchini, jijini Dar es Salaam kuanzia Septemba 4 mwaka huu.
    Mkufunzi wa kozi hiyo itakayofanyika Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume atatoka CAF, na itamalizika Septemba 8 mwaka huu wakati ada ya ushiriki ni sh. 300,000.
    Washiriki wa kozi hiyo ni wale wenye leseni B ya ukocha ya CAF. Fomu kwa ajili ya ushiriki wa kozi hiyo zinapatikana kwenye ofisi za TFF na tovuti ya TFF.
    Mmoja wa makocha wa Ligi Kuu, Freddy Felix Minziro wa JKT Ruvu
    Wakati huo huo: Makocha wa kombaini za mikoa zitakazoshiriki Copa Coca-Cola mwaka 2014 pamoja na waamuzi vijana wa michuano hiyo watashiriki kozi ya ukocha na uamuzi itakayofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Agosti 25 hadi 29 mwaka huu.
    Kozi hiyo itafanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Agosti 25 hadi 29 mwaka huu ikiwa ni sehemu ya maandalizi michuano ya Copa Coca-Cola ngazi ya Taifa itakayochezwa Septemba mwaka huu.
    Makocha watakaoshiriki kozi hiyo na mikoa yao kwenye mabano ni Ahmed Simba (Mwanza), Ally Kagire (Kagera), Aloyce Mayombo (Pwani), Andrew Zoma (Tabora), Anthony Mwamlima (Mbeya), Athuman Kairo (Morogoro), Bakari Ali (Kaskazini Pemba) na Charles Mayaya (Shinyanga).
    Fidelis Kalinga (Iringa), Gabriel Gunda (Singida), Hafidh Muhidin Mcha (Kusini Pemba), Hamis Mabo (Kigoma), John William (Geita), Joseph Assey (Shinyanga), Joseph Haley (Manyara), Jumanne Ntambi (Kilimanjaro), Leonard Jima (Ruvuma), Madenge Omari (Mara), Mohamed Muya (Dodoma), Nicholas Kiondo (Ilala) na Nurdin Gogola (Temeke).
    Osuri Kosuli (Simiyu), Peter Amas (Arusha), Ramadhan Abdulrahman Ramadhan (Mjini Magharibi), Renatus Mayunga (Kinondoni), Samwel Moja (Lindi), Seif Bakari (Katavi), Shaweji Nawanda (Mtwara), Sheha Khamis Rashid (Kaskazini Unguja), Tigana Lukinjo (Njombe), Yusuf Ramadhan Hamis (Kusini Unguja), Zahoro Mohamed (Tanga) na Zakaria Mgambwa (Rukwa).
    Waamuzi vijana watakaoshiriki kozi hiyo chini ya Mkufunzi wa FIFA, Felix Tangawarima wa Zimbabwe ni 33. Kwa upande wa ukocha Mkufunzi ni Ulric Mathiott kutoka Shelisheli.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KOZI YA UKOCHA LESENI A KUFANYIKA SEPTEMBA 4 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top