• HABARI MPYA

    Tuesday, August 19, 2014

    APR YAITOA KWA MATUTA RAYON, KUKUTANA NA POLISI YA RWANDA PIA NUSU FAINALI, KAZI IPO KESHO AZAM NA MERREIKH NYAMIRAMBO

    Na Mahmoud Zubeiry, KIGALI
    POLISI na APR, zote za Rwanda zimekwenda Nusu Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame baada ya kuwatoa wapinzani wao, Atletico ya Burundi na Rayon Sport pia ya Rwanda kwa penalti.
    Baada ya sare ya bila kufungana baina yao na Atletico ndani ya dakika 90, Polisi ilikwenda kushinda kwa penalti 9-8, wachezaji wote 22 wakipiga hadi makipa.
    Mchezo baina ya wapinzani wa jadi hapa Rwanda, APR na Rayon ulimalizika kwa sare ya 2-2 ndani ya dakika 90.
    APR walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 12 mfungaji Ndahinduka Michel kabla ya Rayon kusawazisha kupitia kwa Yossa Bertrand  dakika ya 39 na kupata la pili dakika ya 45 na ushei, mfungaji Ndayisenga Fuad.
    Mugiraneza Jean Baptiste akishangilia baada ya kufunga penalti ya ushindi ya APR

    APR ilikwenda mapumziko ikiwa nyuma kwa mabao 2-1, lakini kipindi cha pili ikarudi kwa nguvu na kufanikiwa kusawazisha dakika ya tano tu tangu kuanza kipindi hicho, mfungaji Rubwiro Herve.
    Baada ya hapo, timu hizo zilianza kushambuliana kwa zamu, kila upande ukisaka bao la ushindi- lakini hadi refa Muhabi Alex wa Uganda anahitimisha mchezo huo, matokeo yalibaki 2-2. 
    Wachezaji wote waliopiga penalti za kwanza walikosa, akianza Tubane James wa Rayon na baadaye, Nshutinamagara Ismael wa APR.
    Baadaye kila upande ukafunga penalti tatu mfululizo zilizofuata, upande wa Rayon zikipigwa na Kembele Gentil Salita, Sibomana Abouba na Mutombo Govin.
    Kwa upande wa APR waliopiga penalti hizo tatu walikuwa ni Mukunzi Yannick, Tibingana Charles na Rutanga Erick. 
    Katika penalti za mwisho, Nahodha Ndayisenga Fuad alikosa mkwaju wa Rayon kabla ya Mugiraneza Jean Baptiste kuifungia penalti ya ushindi APR na kuipeleka Nusu Fainali ya michuano ya mwaka huu.
    Beki wa APR, Rubwiro Herve akiupitia mpira miguu mwa winga wa Rayon, Gueli Koffi leo Nyamirambo

    Kwa matokeo hayo, APR na Polisi zitakutana katika Nusu Fainali- hiyo ikimaanisha tayari Rwanda imeingiza timu fainali.
    Robo Fainali zinatarajiwa kuendelea kesho, mchezo wa kwanza kati ya Azam FC ya Tanzania Bara na El Merreikh ya Sudan na baadaye KCC ya Uganda na Atlabara ya Sudan Kusini.  
    Wachezaji wa Polisi kulia na wa Atletico kushoto wakigombea mpira wa juu. Dakika 90 ziliisha 0-0. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: APR YAITOA KWA MATUTA RAYON, KUKUTANA NA POLISI YA RWANDA PIA NUSU FAINALI, KAZI IPO KESHO AZAM NA MERREIKH NYAMIRAMBO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top