• HABARI MPYA

    Friday, July 18, 2014

    KIPA SIMBA SC ABWAGA MANYANGA

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    KIPA  wa zamani wa kimataifa wa Tanzania na klabu ya Simba, Mwarami Mohammed ‘Shilton’ amestaafu soka na sasa anataka kuwa kocha.
    Mwarami mwenye umri wa miaka 35, amesema kwamba ameona bora kutungika glavu zake kwa heshima kwa sababu umri umeenda.
    “Nimecheza kwa muda mrefu, tangu mwaka 1997 nacheza Ligi Kuu, ni miaka mingi na ninaona mwili umechoka. Ni wakati wa kupumzika kwa heshima sasa,”amesema.
    Mwarami Mohamed amestaafu soka

    Mwarami amestaafu akiwa anachezea Ferroviario de Maputo ya Msumbiji ambayo alijiunga nayo baada ya kuchezea Ferroviario za Pemba na Nampula.
    Kabla ya kwenda Msumbiji, nchini Tanzania, Mwarami alichezea timu za Coastal Union ya Tanga, Simba SC ya Dar es Slaam, Kariakoo United ya Lindi na Reli Morogoro.
    “Nataka kuwa kocha, nimeanza kuafuatilia vyuo vya kwenda kusomea ukocha, lakini kwanza nitapata kozi za awali hapa hapa nchini kwa kuanzia,”alisema.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KIPA SIMBA SC ABWAGA MANYANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top