• HABARI MPYA

    Saturday, April 19, 2014

    YAYA TOURE ATOA YA MOYONI, ASEMA WEUSI NI WANYAMA ULAYA, KUHUSU MESSI NA RONALDO...

    KIUNGO wa Manchester City na Ivory Coast, Yaya Toure anaamini haheshimiki kama mmoja wa wanasoka bora duniani kwa sababu ni Mwafrika.
    Toure amefunga mabao 22 msimu huu, akiisaidia City kushinda Kombe la Ligi na kuendelea kuwamo katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya England.
    Mchezaji mwenzake wa City, Samir Nasri amesema Toure angefurahia kama mmoja wa viungo bora duniani kama asingekuwa Mwafrika.

    Hana furaha: Yaya Toure amesema hachukuliwi kama mmoja wa wachezaji bora duniani kwa sababu ya Uafrika wake

    Alipoulizwa nini anachofikiria, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30, Toure alisema: "Nafikiri kitu alichosema Samir ilikuwa ni ukweli kabisa,".
    Katika mahojiano maalum na Football Focus ya BBC World News, Toure alisema anafikiri hajapata heshima ya kutosha kulingana na mafanikio yake.
    Toure ametwaa mataji ya Ligi Kuu katika nchi nne alizocheza - Ivory Coast, Ugiriki, Hispania na England - na alikuwemo kwenye kikosi cha Barcelona kilichotwaa Kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2009.
    "Kwa kweli, heshima haswa inakuja kutoka kwa mashabiki,"alisema Mwanasoka huyo bora Afrika mara tatu. "Sitaki kuwa mgumu na sitaki kuwa tofauti, lakini nataka kuwa mkweli,".
    Toure anafikiri vyombo vya habari vinapaswa kuwapromoti zaidi wanasoka wa Afrika.
    "Ikiwa tunacheza vizuri na hatupati heshima kwenye vyombo vya habari, hatuwezi kufika tunapotaka,"alisema. "Watu wanachukuliwa watu wa Afrika kama wanyama,". 
    Recognised: Toure was declared the CAF African Footballer of the Year in Nigeria earlier this year
    Heshima: Toure alikabidhiwa tuzo ya Mwanasoka Bora Afrika wa Mwaka mapema mwaka huu nchini Nigeria
    Primed and ready: The languid midfielder will be Ivory Coast's lynchpin during this summer's World Cup
    Mtu babu kubwa: Kiungo huyo anatarajiwa kuiongoza Ivory Coast katika Fainali za Kombe la Dunia
    Strong words: Samir Nasri claims Toure would be considered as one of the best if he wasn't African
    Maneno mazito: Samir Nasri amesema Toure angechukuliwa kama mmoja wa viungo bora duniani iwapo asingekuwa Mwafrika
    Contrast: Toure isn't happy that Lionel Messi is said to be the best but players like himself are overlooked
    Kivuli: Toure hana furaha kama ambayo anayo Lionel Messi anayepewa heshima ya mmoja wa wanasoka bora duniani

    Another trophy: Real Madrid's Cristiano Ronaldo, pictured with the Copa del Rey, won the Ballon d'Or
    Taji lingine: Mchezaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo akiwa ameshika Copa del Rey, naye ameshinda Ballon d'Or mbili
    Toure pia anafikiria wachezaji wa Afrika wanatakiwa kufanya makubwa zaidi ili kulinganishwa na viungo wa Barcelona, Andres Iniesta na Xavi, ambao wote ni wachezaji wenzake wa zamani.
    Amesema Iniesta na Xavi wanapewa heshima kubwa viungo mahiri wa ushambuliaji, lakini huwa hawashutumiwi wanapochemsha uwanjani.
    Toure amesema amekuwa akisakamwa na vyombo vya habari anaopofanya makosa uwanjani. Nyota huyo wa Ivory Coast pia hafurahii kwamba Lionel Messi na Cristiano Ronaldo wanapewa heshima kubwa kama wanasoka bora duniani peke yao, wakati wachezaji wengine kama wao hawapewi heshima hiyo.
    "Ikiwa utaenda sehemu yoyote ya Afrika kwa sasa, watu watakuambia "ndiyo, tunamjua yeye [Messi]", lakini ukija Ulaya na useme 'Yaya Toure' watu watakuambia 'ni nani huyo?' Baadhi watakuambia wanalijua jina langu, lakini hawaijui sura yangu. Lakini wataijua sura ya Messi,"alisema.
    Toure, ambaye amecheza Ubelgiji, Urusi, Ugiriki, Ufaransa, Hispania na sasa England, amesema atastaajabu sana kama hatatajwa Mchezaji Bora wa Mwaka na Chama cha Wanasoka wa kulipwa (PFA). 
    Ni kati ya wachezaji sita walioingia kwenye orodha ya mwisho, sambamba na Eden Hazard wa Chelsea, Adam Lallana wa Southampton na wachezaji watatu wa Liverpool, Luis Suarez, Steven Gerrard na Daniel Sturridge.
    Asked if he would be unhappy not to win the award, Toure replied: 'Definitely. As a champion, as a winner, I always want to win.'
    Only man to clinch it: Former AC Milan striker George Weah is the solitary African winner of the Ballon d'Or
    Mweusi pekee aliyeshinda: Mshambuliaji wa zamani wa AC Milan, George Weah ni Mwafrika pekee aliyeshinda Ballon d'Or
    Lethal finisher: Toure says Chelsea striker Samuel Eto'o is 'more than a legend' in his mind
    Mmaliziaji hodari: Toure amesema mshambuliaji wa Chelsea, Samuel Eto'o ni zaidi ya gwiji kwa mtazamo wake
    Winners! Manchester City clinched the Premier League title under Roberto Mancini in the 2011/12 season
    Washindi! Manchester City wakiwa na taji la ubingwa wa Ligi Kuu ya England chini ya kocha Roberto Mancini msimu wa 2011/12 
    Look at that! Toure inspects the Champions League trophy with Pep Guardiola while at Barcelona in 2009
    Angalia hii! Toure akikagua Kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya na kocha Pep Guardiola wakati walipokuwa Barcelona mwaka 2009

    Alipoulizwa juu ya Mwafrika mmoja tu kushinda Ballon d'Or hadi sasa- mshambuliaji wa zamani wa AC Milan na Liberia, George Weah mwaka 1995 - Toure alielezea pia mambo makubwa yaliyofanywa na wanasoka wengine wa Afrika, Samuel Eto'o na Didier Drogba katika ngazi ya klabu.
    "Hao wachezaji ni zaidi ya magwiji kwangu na kwa Afrika," alisema.
    Alipoulizwa kwamba wachezaji kama Eto'o na Drogba pia wanahisi hawapewi heshima wanayostahili, mchezaji huyo wa zamani wa Barcelona alijibu: "Kabisa".
    Aliongeza: "Najivunia kuwa Mwafrika, nataka kuwatetea watu wa Afrika na ninataka kuionyesha dunia kwamba wachezaji wa Afrika wanaweza kuwa wazuri kama wa Ulaya na Amerika Kusini,".
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YAYA TOURE ATOA YA MOYONI, ASEMA WEUSI NI WANYAMA ULAYA, KUHUSU MESSI NA RONALDO... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top