• HABARI MPYA

    Sunday, April 13, 2014

    MO DEWJI ATOA NASAHA NZITO SIMBA SC

    Na Baby Akwitende, Dar es Salaam
    ALIYEWAHI kuwa mfadhili wa Simba SC, Mohamed ‘Mo’ Dewji amewataka wanachama wa klabu hiyo kuwa makini katika mchakato wa uchaguzi ujao, kuhakikisha wanapata viongozi bora watakaorejesha heshima ya timu.
    Mo ameiambia BIN ZUBEIRY kwamba ni vyema katika wakati mgumu Simba SC ikahakikisha inawekeza katika kuteua viongozi bora ambao wataikwamua timu.
    “Ndugu zangu wanachama wenzangu wa Simba SC, nawaomba sana tuwe makini katika uchaguzi Mkuu ujao, tuhakikishe tunachagua watu ambao wataisaidia timu,”alisema.
    Mohamed Dewji akiwahutubia wapenzi wa Simba SC mwaka 2003 baada ya mapokezi ya timu hiyo ikitokea Misri ambako iliitoa Zamalek.

    Uchaguzi wa Simba umepangwa kufanyika Mei 4, mwaka huu lakini kutokana na kutokamilika kwa usajili wa Katiba hiyo, kuna uwezekano usifanyike kama ilivyopangwa.
    Mo Dewji, mmoja wa wafanyabiashara wakubwa na wenye kuheshimika barani Afrika alikuwa mfadhili wa klabu hiyo tangu mwaka 1999 hadi 2005 alipoamua kujiweka kando.
    Katika kipindi cha ufadhili wake, Simba SC ilipata mafanikio kiasi cha kufikia kucheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ikiitoa Zamalek ya Misri iliyokuwa bingwa mtetezi mwaka 2003. 
    Wanachama wengi wa Simba SC wana hamu Mo Dewji arejee katika klabu hiyo kuongeza nguvu, kwani kwa sasa kwa kiasi kikubwa inamtegemea Zacharia Hans Poppe.
    Inawezekana Mo Dewji akarejesha fedha zake Simba SC haswa baada ya kuachana na timu aliyokuwa anaimiliki, African Lyon.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MO DEWJI ATOA NASAHA NZITO SIMBA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top