MAN CITY YAIFUMUA TENA CHELSEA MAREKANI, SAFARI HII YAIPIGA 'MKONO'


IMEWEKWA MEI 26, 2013 SAA 2:00 ASUBUHI
KLABU ya Manchester City imeitandika mabao 5-3 Chelsea katika mchezo wao wa pili na wa mwisho kwenye ziara yao ya Marekani jana kwenye Uwanja wa St Louis baada ya Alhamisi pia kushinda 4-3 kwenye Uwanaj huo huo dhidi ya The Blues. 
Mabao ya City yalifungwa Barry dakika ya tatu, Nasri dakika ya 29 na 73, Milner dakika ya 54 na Dzeko dakika ya 84, wakati wa Chelsea yalifungwa na Ramires dakika ya 48 na 68 na Mata dakika ya 82. 
Kikosi cha Man City kilikuwa: Hart/Wright dk45,, Zabaleta/Maicon dk45, Kompany/Lescott dk45, Boyata/Garcia dk55, Kolarov, Yaya Toure/Rodwell dk45, Barry, Nasri, Tevez/Razak dk45, Silva/Milner dk45 na Aguero/Dzeko dk45.
Chelsea: Hilario/Cech dk45, Azpilicueta, Christensen, Luiz/Mata dk61, Ake, Mikel, Loftus-Cheek/Ferreira dk42, Ramires, Oscar/Benayoun dk65, Ba na Torres.
Rampage: Man City won their second high-scoring game against Chelsea in a couple of days
Wachezaji wa Man City wameshinda tena dhidi ya Chelsea jana
Drafted: Samir Nasri, who was the star of the show, lifts the ball over Petr Cech
Samir Nasri akimfunga Petr Cech
Dead on: Juan Mata's precise free-kick which curled into the top corner wowed the crowd
Juan Mata akifunga kwa mpira wa adhabu

ROONEY AITWA FARAGHA NA MOYES ATULIZWE ABAKI MAN UNITED


IMEWEKWA MEI 26, 2013 SAA 1:40 ASUBUHI
MSHAMBULIAJI Wayne Rooney anatarajiwa kuwa kikao maalum na kocha mpya wa Manchester United, David Moyes kama sehemu ya juhudi za klabu kutatua tatizo la nyota huyo wa England juu ya mustakabali wake baada ya kutofautiana na kocha aliyeondoka, Sir Alex Ferguson. 
Wakati Moyes anajiandaa kwa sikukuu ya kifamilia na Rooney yupo kwenye majukumu ya timu ya taifa ya England  wiki hii, inafahamika kwamba wote wapo tayari kukutana haraka iwezekanvyo kutatua mustakabali wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27, Rooney. 
Klabu sasa imekubali Rooney hajawahi kutoa maombi ya kuondoka na pamoja na hayo, Moyes atataka kukutana na mchezaji huyo binafsi kabla ya uamuzi wa mwisho kufikiwa. Rooney anataka kubaki katika klabu hiyo na Moyes anamkubali mchezaji huyo. 
Ringside: Manchester United striker Wayne Rooney was at the O2 Arena on Saturday night
Pembeni ya ulingo: Mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney alikuwa kwenye Uwanja wa O2 Arena jana usiku kuangalia ndondi
Wayne Rooney
David Moyes
Makofi: Wayne Rooney atakutana na David Moyes kujadili mustakabali wake Manchester United

NEYMAR AIKATAA REAL MADRID, KUSAINI MIAKA TANO NA BARCELONA KESHO


IMEWEKWA MEI 26, 2013 SAA 1:00 ASUBUHI
MABINGWA wa Hispania, Barcelona wamekubali kumsajili mshambuliaji wa Brazil, Neymar kutoka klabu ya Santos.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 21, atasaini mkataba wa miaka mitano, klabu hiyo imesema na mchezaji mwenyewe amethibitisha atasaini kesho.
Taarifa ya Barcelona imesema: "FC Barcelona na Santos zimekubaliana kuhusu Neymar da Silva Santos Junior. Mshambuliaji wa Kibrazil atakuwa mchezaji wa Blaugrana  kwa miaka mitano ijayo. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 ni miongoni mwa wachezaji wanaochipukia vizuri duniani.'
Heading off: Neymar left a heartfelt message for the fans of FC Santos
Anaondoka: Neymar anaondoka na chini ni ujumbe alioandika kwa ajili ya mashabiki wa FC Santos
Neymar's message

Neymar alilazimika kuamua mustakabali wake, baada ya klabu yake, Santos kusema Ijumaa kwamba wamepokea ofa mbili kwa ajili ya nyota huyo na Barca ikathibitika kuwa ni moja ya klabi zilizotoa ofa huku, Real Madrid ikidhaniwa kuwa ni klabu nyingine.
Neymar am,ethibitisha uamuzi wake kwa kuandika kwenye Instagram: "Nipo hapa na marafiki na familia na wananisaidia kuandika vitu vichache hapa. Siwezi kusema hadi Jumatatu. Familia yangu na rafiki zangu tayari wanajua uamuzi wangu.
Jumatatu nitasaini mkataba na Barcelona,".'
Mkataba wake na Santos unatarajiwa kumalizika msimu ujao na baadhi ya taarifa zinasema kwamba makubaliano na Barcelona yalifikiwa mwaka mmoja uliopita.
Neymar atawaaga mashabiki wa Santos katika mchezo wa leo wa ufunguzi wa msimu dhidi ya Flamengo.
Home hero: Neymar (right) has spent his whole career at Santos and has won 32 caps for his country
Anafuata nyayo: Neymar (kulia) amekuwa akiichezea Santos muda wote na ameichezea timu ya taifa ya Brazil mechi 32. Hapa yupo na Mwanasoka Bora wa zamani wa dunia, Mbrazil mwenzake, Ronaldinho, aliyewahi kung'ara Barcelona.

RAIS KIKWETE AMEWAPA CHANGAMOTO NZURI TFF, WAIFANYIE KAZI


IMEWEKWA MEI 26, 2013 SAA 12:30 ASUBUHI
ALHAMISI wiki hii, RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete aliwaalika Ikulu wachezaji wa timu ya soka ya taifa, Taifa Stars na akazungumza nao mambo kadhaa, kubwa kuwahamasisha katika kampeni yao ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia, mwakani nchini Brazil.
Ikumbukwe, hadi sasa, Stars inashika nafasi ya pili katika Kundi C, ikiwa na pointi sita baada ya kucheza mechi tatu kushinda mbili na kufungwa moja, nyuma ya Ivory Coast yenye pointi saba, iliyoshinda mechi mbili na kutoa sare moja.

Kama Stars itashinda mechi yake ijayo ugenini dhidi ya Morocco, Juni 8, mwaka huu itajiweka katika nafasi nzuri ya kuingia kwenye hatua ya mwisho ya kuwania tiketi ya Brazil.
Ikifanikiwa kumaliza kileleni kwa Kundi hilo, lenye timu za Ivory Coast, Morocco na Gambia pia, Stars itacheza mechi mbili za mwisho nyumbani na ugenini dhidi ya moja ya timu zitakazoongoza makundi  na ikishinda itaweka historia ya kucheza Fainali za Kwanza za Kombe la Dunia.
Stars, imekuwa na mwenendo mzuri chini ya Mdenmark Kim Pouslen, ambaye ameiwezesha kushinda mechi tano kati ya 10, sare tatu na kufungwa mbili tangu aanze kazi Mei mwaka jana, akirithi mikoba ya Mdenmark mwenzake, Jan Poulsen.
Hakika mwenendo huo umemvutia Rais Kikwete na wiki hii akaona vema akutane na vijana kabla hawajaenda Morocco kucheza mechi yao ya kwanza ya mzunguko wa pili. Mheshimiwa Rais alisema mengi kiasi fulani, akiwaahidi wachezaji wa timu hiyo kuwafanyia kitu kizuri ambacho kitakuwa kumbukumbu nzuri katika maisha yao, iwapo wataongoza Kundi C. 
Lakini pamoja na hayo, Rais Kikwete alizungumzia mustakabali mzima wa timu hiyo na akalitaka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kujenga uwezo wa kuwalipa makocha wa Taifa Stars, ili Serikali inayotekeleza jukumu hilo kwa sasa, ifikie wakati ijivue mzigo huo.
Alisema kwamba Serikali imelazimika kuendelea kulipa mishahara ya makocha wa timu ya taifa, kwa sababu bado TFF hawana uwezo wa kufanya hivyo.
Hata hivyo, Rais Kikwete alimtaka Rais wa TFF, Leodegar Chillah Tenga kuhakikisha wanajenga uwezo wa kulipa maocha wa timu hiyo na kuipunguzia mzigo huo Serikali.
Rais Kikwete alianza kugharamia mishahara ya makocha tangu alipoingia Ikulu mwaka 2005 na mwalimu wa kwanza alikuwa ni Mbrazil Marcio Maximo aliyeanza kazi Juni mwaka 2006 nchini, akafuatiwa na Mdenmark, Jan Borge Poulsen mwaka 2010 na sasa Mdenmark mwingine, Kim Poulsen aliyeanza kazi Mei mwaka jana.
Kwa kweli wapenzi wa soka nchini wana kila sababu ya kumshukuru Rais Kikwete, kwa kazi kubwa aliyoifanya katika kujenga ustawi mpya wa timu ya taifa, kwani hali ilikwishakuwa mbaya na timu hiyo ilipoteza mvuto na hadhi yake, kaisi hata cha wachezaji kutokuwa na hamu nayo.
Lakini leo kila mchezaji anataka kuchezea timu ya taifa na hata klabu zinapenda kuona wachezaji wao wanaitwa Taifa Stars. Hii imetokana na juhudi za dhati za Rais Kikwete tangu ameingia Ikulu mwaka 2005, kujitolea kusaidia kwa hali na mali ustawi mpya wa timu hiyo.
Leo Taifa Stars ina ufadhili mnono wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Kilimanjaro, inashiriki mashindano kwa uhakika na ndiyo maana hata nguvu ya kupambana kwa ajili ya nafasi inapatikana.
Lakini pamoja na ukweli huo wa msaada wa Rais, hatupaswi kusahau kwamba soka ni mchezo ambao unasimamiwa na taasisi maalum na hiyo si nyingine, bali TFF. Lazima ufike wakati, taasisi hiyo kama ilivyojipa mamlaka kamili ya kusimamia mambo yake, bila kuingiliwa hata na dola, basi iweze kujimudu kwa kila hali.
Umefika wakati tuone faida ya kuwa na viongozi wasomi katika soka yetu kwa kuonyesha weledi na ubunifu wao, kwa kuifanya soka ya Tanzania iweze kujidumu kupitia taasisi yake na kuepuka kutegemea misaada.
Suala kama mshahara wa kocha, kama TFF iliingia Mkataba wa udhamini na TBL, je haikujua kwamba timu itahitaji kuwa na kocha, ambaye atahitaji bajeti maaalum ya kuwepo kwake nchini kufanya kazi? Na mbona mishahara ya makocha inaendelea kuwa mzigo wa Serikali?
Watu hawawezi kupinga Serikali kusaidia michezo, lakini kuna maeneo mengi ambayo Serikali inahitajika, tena kwa dhati kutia mkono wake, lakini si kwa timu ya taifa ambayo kwa sasa inaonekana kabisa kuogelea kwenye bwawa la udhamini mnono wa TBL.
Pamoja na yote, suala la makocha, nchi nyingi hapa hapa kwetu Afrika, tena ukanda huu huu wa CECAFA, makocha wanalipwa na vyama vya soka vya nchi husika- kwa nini TFF inashindwa kufanya hivyo?
Tuache kuishi kwa mazoea, kwamba eti hata wakati Mwalimu Julius Nyerere makocha wa Stars walikuwa walikuwa wanalipwa na Serikali- hapana, lazima tukubali kubadilika kwa ujumla. 
Rais JK amewapa changamoto nzuri TFF, waifanyie kazi. Umefika wakati wajenge uwezo wa kujidumu kikamilifu. Jumapili njema.     

ROBBEN AIBEBESHA UBINGWA WA ULAYA BAYERN KWA BAO LA DAKIKA YA 89 WEMBLEY


Top of the pile: Bayern Munich are the Champions of Europe for a fifth time after beating Borussia Dortmund
Mabingwa: Bayern Munich wakisherehekea taji lao la Ligi ya Mabingwa baada ya kuifunga Borussia Dortmund
Top of the pile: Bayern Munich are the Champions of Europe for a fifth time after beating Borussia Dortmund
Top of the pile: Bayern Munich are the Champions of Europe for a fifth time after beating Borussia Dortmund
Top of the pile: Bayern Munich are the Champions of Europe for a fifth time after beating Borussia Dortmund

IMEWEKWA MEI 25, 2013 SAA 6:00 USIKU
WINGA Arjen Robben ameuzika mzimu wa kukosa penalti msimu uliopita katika fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Chelsea, baada ya usiku huu kuifungia bao la ushindi Bayern Munich katika fainali ya michuano hiyo Uwanja wa Wembley, London, England ikishinda 2-1 na kutwaa Kombe hilo.
Bayern sasa wanakuwa mabingwa wapya wa Ulaya, wakirithi taji lililoachwa wazi na Chelsea kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Wajerumani wenzao, Borussia Dortmund katika mchezo mkali na wa kusisimua.
Mholanzi huyo alifunga bao hilo tamu dakika ya 89, baada ya awali kipindi cha kwanza kukosa mabao mawili ya wazi. Lakini ndiye aliyetoa pasi ya bao la kwanza kwa Bayern lililofungwa na Mario Mandzukic dakika ya 60.
Dortmund ilisawazisha kwa penalti baada ya Dante kumuangusha kwenye eneo la hatari Marco Reus na Ilkay Gundogan akaenda kufunga dakika ya 67. 
Katika mchezo huo, uliochezeshwa na refa Nicola Rizzoli  kutoka Italia, kikosi cha Bayern kilikuwa; Neuer, Lahm, Boateng, Dante, Alaba, Javi Martinez, Schweinsteiger, Robben, Muller, Ribery/Gustavo dk90+1 na Mandzukic/Gomez dk90+4.  
Borussia Dortmund: Weidenfeller, Piszczek, Subotic, Hummels, Schmelzer, Bender/Sahin dk90+1, Gundogan, Blaszczykowski/Schieber dk90+1, Reus, Grosskreutz na Lewandowski.  
Dutch delight: Arjen Robben settled the Champions League final with a late, late strike
Bao la ubingwa: Arjen Robben amekuwa shujaa wa fainali ya Ligi ya Mabingwa usiku huu
Dutch delight: Arjen Robben settled the Champions League final with a late, late strike
Big chances: The first-half was the tale of two goalkeepers with Roman Weidenfeller denying Arjen Robben, and Manuel Neuer keeping Robert Lewandowski out
Champions League final
Champions League final
Controversy: Franck Ribery was lucky to escape punishment when his flailing arm caught Lewandowski in the face
Controversy: Franck Ribery was lucky to escape punishment when his flailing arm caught Lewandowski in the face
Controversy: Franck Ribery was lucky to escape punishment when his flailing arm caught Lewandowski in the face
Breakthrough: Robben finally wriggled free to set up Mario Mandzukic for the opener in the second half

AGUERO AJITIA PINGU HADI 2017 MAN CITY


IMEWEKWA MEI 25, 2013 SAA 5:50 USIKU
MSHAMBULIAJI Sergio Aguero amesaini mkataba wa kuendelea kuichezea Manchester City hadi mwaka 2017.
Mshambuliaji huyo mwenye kipaji, mmoja wa walio bora duniani, amekuwa akiwaniwa na Real Madrid kwa ajili ya msimu ujao baada ya kufanya kazi nzuri Etihad, lakini ameamua kujitia pingu kabla hata ya kuajiriwa kwa kocha mpya.
"Nina furaha sana City na ninahisi nakubalika sana,"alisema.
Crucial: Sergio Aguero is among the Premier League's best players
Sergio Aguero

KIKOSI CHA TIMU YA TAIFA WANAWAKE CHATAJWA

Kocha Kaijage

Na Boniface Wambura, IMEWEKWA MEI 25, 2013 SAA 5:01 USIKU
KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya wanawake ya mpira wa miguu (Twiga Stars), Rogasian Kaijage amewaita kambini wachezaji 30 ikiwa ni mwendelezo wa kuijenga na kuiimarisha timu hiyo.
Twiga Stars itakuwa na kambi ya siku kumi kuanzia Jumapili (Mei 26 mwaka huu) ambapo baadaye inatarajia kucheza mechi moja ya kirafiki kabla ya wachezaji kurudi kwenye klabu zao.
Kambi hiyo ni mwendelezo wa programu iliyopendekezwa na kocha kuijenga na kuiimarisha timu hiyo kwa vile haina mashindano mwaka huu, na itakuwa kambi ya pili baada ya ile iliyofanyika Machi mwaka huu.
Wachezaji walioitwa na klabu zao kwenye mabano ni Asha Rashid (Mburahati Queens), Aziza Mwadini (Zanzibar), Belina Julius (Lord Barden), Ester Chabruma (Sayari), Ester Mayala (TSC Academy), Eto Mlenzi (JKT), Evelyn Sekikubo (Mburahati Queens) na Fatuma Bushiri (Mburahati Queens).
Fatuma Hassan (Mburahati Queens), Fatuma Omari (Sayari), Flora Kayanda (Tanzanite), Hamisa Athuman (Marsh Academy), Hellen Peter (JKT), Maimuna Said (JKT), Mwajuma Abdallah (Tanzanite), Mwanahamisi Omari (Mburahati Queens), Mwanaidi Tamba (Mburahati Queens) na Mwapewa Mtumwa (Sayari).
Nabila Ahmed (Marsh Academy), Pulkeria Charaji (Sayari), Rehema Abdul (Lord Barden), Rukia Khamis (Uzuri Queens), Semeni Abeid (Tanzanite), Sharida Boniface (Makongo Sekondari), Sophia Mwasikili (Sayari), Therese Yona (TSC Academy), Vumilia Maarifa (Evergreen) na Zena Khamis (Mburahati Queens).

TIMU YA KALI ONGALA YAKIPIGA LIGI YA MABINGWA

Kali Ongala aliibukia Abajalo

Na Boniface Wambura, IMEWEKWA MEI 25, 2013 SAA 5:00 USIKU
RAUNDI ya pili ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) inaendelea kesho (Mei 26 mwaka huu) kwa mechi sita za kwanza zitakazochezwa katika miji sita tofauti.
Abajalo ya Sinza, Dar es Salaam iliyomuinua Kocha Msaidizi wa Azam FC, Kali Ongala akasajiliwa Yanga SC mwaka 1999 kabla ya kwenda kucheza soka ya kulipwa Amerika na Ulaya, itamenyana na na Kariakoo ya Lindi kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam wakati Machava FC ya Kilimanjaro itakuwa mwenyeji wa Mpwapwa Stars ya Dodoma kwenye Uwanja wa Ushirika mjini Moshi.
Nayo Stand United FC ya Shinyanga itakuwa mgeni wa Magic Pressure ya Singida kwenye Uwanja wa Namfua mjini Singida huku Polisi Jamii ya Bunda mkoani Mara ikimenyana na Biharamulo FC ya Kagera kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma.
Mjini Kigoma kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika ni kati ya wenyeji Saigon FC na Katavi Warriors ya Katavi wakati Njombe Mji itaikaribisha Kimondo SC ya Mbeya kwenye Uwanja wa Sabasaba mjini Njombe.
Leo (Mei 25 mwaka huu) Friends Rangers ya Kinondoni, Dar es Salaam inacheza na African Sports ya Tanga kwenye Uwanja wa Azam Chamazi. Mechi za marudiano zitachezwa kati ya Juni 1 na 2 mwaka huu.
Timu zitakazofuzu kucheza raundi ya tatu zitacheza mechi za kwanza kati ya Juni 8 na 9 mwaka huu wakati mechi za marudiano zitakuwa kati ya Juni 15 na 16 mwaka huu.

WACHEZAJI TAIFA STARS WAPIGILIA 'SUTI ZA KUFA MTU' NA KUFANYA BONGE LA SHOO LA MAVAZI JUKWAANI USIKU HUU

IMEWEKWA MEI 25, 2013 SAA 4:30 USIKU
Wachezaji wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars wakiwa vazi maalum la suti katika hoteli ya Hyatt, zamani Kilimanjaro Kempinski usuku huu ambazo watavaa katika safari ya Morocco watakapokwenda kumenyana na wenyeji, Simba wa Atlasi kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia mwakani nchini Brazil.

Simon Msuva kulia na Mrisho Ngassa kushoto wakipita jukwaani kwa madaha na vazi hilo katika hafla maalum ya kutambulisha vazi hilo, iliyoandaliwa na wadhamini wa timu hiyo, Kilimanjaro Premium Lager, bia inayozalishwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL)

Hawa walivaa suti za kimichezo

Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa TBL, Focus Lasway kulia akimkabidhi suti hizo, Katibu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Angetile Osiah. Wengine pichani ni Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe kulia na Rais wa TFF, Leodegar Tenga kushoto.   

Mkurugenzi wa Executive Solutions Limited, Aggrey Marealle kushoto, Waratibu wa udhamini wa Taifa Stars TBL

Kutoka kulia Katibu wa TFF, Angetile Osiah, Mtangazaji wa EATV, Patrick Nyembela na Mkurugenzi wa Masoko wa TFF, Jimmy Kabwe

Kavishe akizungumza na Mjumbe wa Kamati ya Saidia Taifa Stars Ishinde, Teddy Mapunda 

Baadhi wa Waandishi wa Habari waliohudhuria hafla hiyo

Kocha wa makipa wa Taifa Stars, Juma Pondamali akipita jukwaani kwa madaha kuonyesha vazi la suti ya kimichezo

Msanii Barnaba akiimba wimbo wa taifa katika uzinduzi wa vazi hilo

Wachezaji katika picha ya pamoja na vimwana

Kicheko; Kevin Yondan kulia na Shomary Kapombe kushoto wakifuarahia jambo

Kutoka kulia Shomary Kapombe, Juma Kaseja na Zahor Pazi

Kutoka kulia Juma Kaseja, Angetile Osiah, Salim Mohamed wa Friends Of Simba na Zahor Pazi  

Mwaa!; Kimwana akimpiga busu Mrisho Ngassa

Handsome; Kevin Yondan

Nadir Cannavaro na kimwana

Amri Kiemba kulia na Aggrey Morris

Kutoka kulia Athumani Iddi 'Chuji', kocha Kim Poulsen na Mwinyi Kazimoto 

Meneja Leopold Mukebezi kulia na kocha Kim Poulsen kushoto 

Kutoka kulia Mwinyi Kazimoto, Athumani Iddi na Salum Abubakar 'Sure Boy'

Kutoka kulia Frank Domayo, John Bocco, Erasto Nyoni na Khamis Mcha

John Bocco kulia na Erasto Nyoni kushoto

BREAKING NEWS; SIMBA SC YASAJILI WATATU KWA MPIGO...KIPA, BEKI NA MSHAMBULIAJI HATARI WA TAIFA STARS

Kimya kimya; Mwenyekiti wa kamati ya Usajili Simba SC, Zacharia Hans Poppe 

Na Mahmoud Zubeiry, IMEWEKWA MEI 25, 2013 SAA 5:20 ASUBUHI
SIMBA SC usiku wa jana imesaini wachezaji watatu wapya kwa mpigo, akiwemo mshambuliaji hatari wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Zahor Iddi Pazi ambaye msimu uliopita alikuwa anatakiwa na Yanga SC akatimkia Azam FC.
Ametua Msimbazi; Zahor Pazi

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe ameaimbia BIN ZUBEIRY leo kwamba, mbali na Zahor anayechezea JKT Ruvu kwa mkopo akitokea Azam FC, wengine waliosajiliwa ni kipa Andrew Ntala kutoka Kagera Sugar na beki Issa Rashid ‘Baba Ubaya’ kutoka Mtibwa Sugar.
Poppe, ambaye ni Kapteni wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) alisema wachezaji wote wamesaini mikataba ya miaka miwili kila mmoja.
“Bado tunaendelea na usajili wetu kwa umakini na kimya kimya. Nataka nirudie kusema kwamba, sera ya Simba SC si kusajili kutoka Yanga SC. Bali wao Yanga ndio wanasajili kwetu. 
Nashangaa jana Katibu wao (Lawrence Mwalusako) ametamba ameniziba mimi mdomo baada ya kumsaini Haruna Niyonzima,”.
“Yule ni mchezaji wao, na sisi hatujawahi kutoa tamko la kumtaka yule mchezaji. Kama alikuwa anawatia presha ili wampe fedha nyingi kwa kuwahadaa Simba wanamtaka, amefanikiwa, ila sisi hakuwa kabisa katika mipango yetu,”alisema Poppe.
Poppe amesema Simba SC wanasajili kisayansi na si kama wapinzani wao hao, Yanga SC ambao wanaingia hasara ya fedha nyingi na wanacheza pata potea.
“Sisi tulimsajili Mbuyu Twite kama yeye tu, lakini wao wakaingilia akawapa sharti wamsajili na ndugu yake (Kabange Twite), wakaingia mkenge wakasajili mtu ambaye wamemlipa fedha nyingi, lakini hawajamtumia na hakuwa chaguo lao,”.
Kiboko ya Msuva; Issa Rashid
'Baba Ubaya' ametua Simba SC

“Sasa sisi hatuna ulimbukeni wa aina ile katika kusajili, tunafanya mambo yetu kisayansi, na ndiyo maana wachezaji tunaosajili wanakuwa lulu na baadaye tunawauza nje kwa fedha nyingi tunapata faida kubwa, angalia Patrick Ochan, Emanuel Okwi na Mbwana Samatta. “Biashara nzuri sana. Hatukutumia hata Sh. Milioni 100 katika usajili wao, wameingiza karibu Milioni 700, Yanga wanaweza?”alihoji Poppe.
Poppe alisema pamoja na kusaini watatu hao wapya, Simba SC imewapa mikataba wachezaji wake kadhaa chipukizi waliopandishwa kutoka kikosi cha pili, akiwemo Haruna Chanongo ambaye alikuwa kwenye rada za Yanga pia.
Kusajiliwa kwa watatu hao wapya, kunafanya idadi ya wachezaji wapya waliosajiliwa Simba SC kufika wanne, baada ya Twaha Shekuwe ‘Messi’ wa Coastal Union kuwa mchezaji wa kwanza mpya kusajiliwa katika timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao.
Lakini Simba SC, tayari imempoteza mchezaji mmoja, Mrisho Ngassa ambaye amesajiliwa na watani wa jadi, Yanga SC.